#HABARI: Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) Wilaya ya Mkuranga, mkoani Pwani, imeendelea kuboresha miundombinu ya Barabara kwa kutekeleza miradi mikubwa yenyethamani ya zaidi ya Shilingi Bilioni 22, ikilenga kurahisisha usafiri na kuinua uchumi wa wananchi wa Vijijini na Mijini.
Hayo yamebainishwa na Kaimu Meneja wa TARURA wa Wilaya ya Mkuranga, Mhandisi Silas Dilliwa, na kwamba miradi hiyo ambayo inaendelea na ujenzi katika Wilaya hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa mpango wa Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ambaye kwa sasa ni Mgombea Kiti cha Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) kuboresha barabara kwa maendeleo ya kiuchumi na kijamii.
Wananchi wa Kijiji cha Magawa, pamoja na wananchi wa Mkuranga Mjini, wamesema wanaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita kwa ujenzi wa Miundombinu ya Barabara pamoja na madaraja kwakuwa walikuwa wanapata shida sana hasa kipindi cha mvua.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
📱Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 📱kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
#Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.