Wakati saa zikihesabika kabla ya uchaguzi mkuu wiki hii, mvutano umeibuka kati ya mgombea ueais Zanzibar kwa tiketi ya Chama cha ACT Wazalendo, Othman Masoud Othman na Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) kuhusiana na uendeshaji wa uchaguzi.
Miongoni mwa hoja alizoibua mgombea wa ACT Wazalendo ni pamoja na madai ya wizi wa kura za mapema zinazopigwa kesho na kucheleweshwa kwa matokeo, huku ZEC ikikanusha tuhuma hizo na kusema hazina uthibitisho.
#AzamTVUpdates
Mhariri | John Mbalamwezi