
Mwili wa mateka aliyefariki akizuiliwa katika Ukanda wa Gaza uliwasili nchini Israel Jumatatu jioni baada ya jeshi la Israel kusema kutangaza kuwa Hamas imekabidhi mwili wa mateka kwa Shirika la Msalaba Mwekundu huko Gaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tangu kuafikiwa kwa makubaliano ya kusitishwa kwa mapiganao yalioongozwa na Marekani kati ya Israel na Hamas tarehe 10 Oktoba, miili ya mateka 16 imerejeshwa Israel.
Miili mingine 12 bado inaendelea kutafutwa huko Gaza ili kukabidhiwa kwa mamlaka ya Israel.
Hamas imeongeza kasi ya utafutaji wa miili ya mateka waliofariki katika Ukanda wa Gaza, kulingana na taarifa ya kundi ya siku ya Jumapili ya wiki iliopita, ikiwa imepita siku moja baada ya Misri kutuma timu ya wataalam na vifaa maalum kusaidia katika upatikanaji wa miili hiyo.
Chini ya usitishaji huo wa mapigano Hamas inatarajiwa kurejesha miili ya mateka wote wa Israel waliofariki haraka iwezekanavyo.
Israel imekubali kurejesha miili 15 ya Wapalestina kwa kila mwili mmoja wa Mwisiraeli.