Imechapishwa: Imehaririwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Miili ya wapalestina 41 imezikwa katika kaburi la pamoja katika eneo la Deir al- Balah katika ukanda wa Gaza.

Hii ni kati ya miili 195 ya Wapalestina, iliyorudishwa kwenye ukanda wa Gaza, baada ya mkataba wa usitishwaji wa vita kati ya Israel na kundi la Hamas.

Wapalestina hao waliouawa katika uwanja wa vita vilivyodumu kwa miaka miwili, walipelekwa katika hospitali ya Nasser katika eneo la Khan Younis na kupokelewa na wapendwa wao.

Miili hiyo ni ya Wapalestina waliorejeshwa kutoka Israel.
Miili hiyo ni ya Wapalestina waliorejeshwa kutoka Israel. AP – Jehad Alshrafi

Jeshi la Israel limeliambia Shirika la Habari la A kuwa, miiili yote iliyorejeshwa ni ya wapiganaji wa Hamas, lakini shirika hilo halijathibitisha, ukweli wa maelezo hayo kwa njia ya picha na mikanda ya video.

Aidha, familia za watu hao zimekanusha kuwa wapendwa wao ni wanamgambo wa Hamas.

Katika hatua nyingine, Israeli, imekubali kurejesha miili 15 ya mateka wengine, ambao hata hivyo hawajatambuliwa kwa sababu ukaguzi wa vinasaba, haujafanyika, kuitambua.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *