Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) imesema wananchi wameanza kupiga kura ya mapema leo katika vituo mbalimbali visiwani humo.

Wanaotakiwa kupiga kura hiyo kwa mujibu wa sheria ni pamoja na wafanyakazi wa tume hiyo pamoja na vyombo vya ulinzi na usalama ambao wamepangwa kuendesha zoezi la uchaguzi kesho Oktoba 29.

Mkurugenzi wa ZEC, Thabit idarusi Faina ameongeza kusema kuwa, zoezi zima la uchaguzi linaenda vizuri na ametoa wito kwa wananchi kuendelea kuiamini tume hiyo kwani watafanya kazi kwa uweledi.

✍Juliana James
Mhariri | @claud_jm

#AzamTVUpdates

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *