Dar es Salaam. Mwanamuziki wa Mali, Salif Keita anatarajiwa kukiwasha katika tamasha la Sauti za Busara litalofanyika Februari 5-8, 2026, Zanzibar.

Sauti za Busara wameachia orodha ya wasanii ambao watatumbuiza katika tamasha hilo. Mmoja wapo akiwa Keita ambaye anatajwa kama mmoja wa mwanamuziki mwenye ushawishi mkubwa Barani Afrika.

“Sauti ya Dhahabu ya Afrika inakuja Zanzibar. Nguli Salif Keita, mmoja wa wasanii wenye heshima na ushawishi mkubwa barani Afrika, atapanda jukwaani kwenye tamasha la Sauti za Busara 2026.

Msanii huyo ambaye amekuwa, akichanganya mila na midundo ya kimataifa katika kazi zake zinazohadithia ufahari wa Afrika ataungana na wasanii wengine wa Tanzania kama Ben Pol na Man Fongo.

Katika taarifa hiyo ya Sauti za Busara imeeleza kuwa “Nyimbo zake kama Yamore, Africa, na Tomorrow, muziki wake ni zaidi ya midundo ni harakati, ni kumbukumbu, ni kioo cha roho ya bara letu. Kuwapo kwake Zanzibar ni zaidi ya onyesho ni kusherehekea muziki wa Afrika, urithi wetu na uthabiti wa roho ya bara,” imeeleza 

Wasanii wengine ni Hammer Q, Pilani Bubu, Kara Sylla Ka & Baye Fall Band, Atanda & Afrojazz Messengers, Tarajazz na wengine wengi

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *