Miongoni mwa madhara hayo ni ucheleweshaji au kukosa kabisa huduma za afya na huduma za dharura; kuvurugika kwa shughuli za kibinadamu ikiwemo familia kushindwa kuwasiliana na wengine na kuvurugika kwa shughuli za biashara na benki.

Picha ya angani ya nyumba zilizoharibiwa wakati wa kimbunga Beryl huko Jamaika. (Maktaba)

IOM/Gema Cortes

Picha ya angani ya nyumba zilizoharibiwa wakati wa kimbunga Beryl huko Jamaika. (Maktaba)

Kimbunga Melissa

Mamilioni ya watu nchini Jamaica na katika ukanda wote wa Karibea wanajiandaa kukabiliana na madhara makubwa ya kimbunga Melissa huku Umoja wa Mataifa na washirika wake wakionya kuhusu tishio kubwa na la haraka la kibinadamu.

Akizungumza na waandishi wa habari huko Geneva Uswisi hii leo, Necephor Mghendi, Afisa kutoka shirikisho la Msalaba Mwekundu na Hilal Nyekundu, (IFRC) amesema,

“Takribani watu milioni moja wako hatarini, zikiwemo familia ambazo bado zina madhara ya Kimbunga Beryl. Kumbuka, ni miezi 16 tu imepita. Kimbunga Melissa kinasonga kwa kasi ndogo sana, lakini pia kina uwezo mkubwa wa kuleta mvua nyingi kupita kiasi, mawimbi makubwa ya baharini, na upepo mkali unaoweza kusababisha uharibifu mkubwa wa miundombinu, kutenga jamii na kukatiza huduma muhimu kwa siku kadhaa, labda hata wiki. Tishio la kibinadamu ni kubwa na la haraka.”

Watoto wameketi kando ya hema za muda huko El Fasher, Darfur Kaskazini, ambako mapigano makali yamewaacha maelfu wamenaswa.

Watoto wameketi kando ya hema za muda huko El Fasher, Darfur Kaskazini, ambako mapigano makali yamewaacha maelfu wamenaswa.

Sudan

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, António Guterres, ameelezea wasiwasi wake mkubwa kufuatia kuongezeka kwa mapigano ya kijeshi mjini El Fasher, jimbo la Darfur Kaskazini, nchini Sudan. Kupitia taarifa iliyotolewa na Msemaji wake usiku wa tarehe27 Oktoba 2025 kwa saa za New York marekani, Guterres amesema kwa zaidi ya miezi kumi na minane, wakazi wa El Fasher na maeneo ya jirani wamekuwa wakikabiliwa na mateso makubwa huku makundi ya Wanamgambo wa Rapid Support Forces (RSF) yakizingira mji huo.

Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi, UNHCR hii leo limesema maelfu ya watu wamekimbia mji huo huku wengine wengi wakisalia wamenasa ndani bila kujua la kufanya, hofu ikiwa imewagubika.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *