
Nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), utawala wa Rais Félix Tshisekedi unavichukulia hatua kali vyama 12 vya upinzani. Naibu Waziri Mkuu anayehusika na Mambo ya Ndani na Usalama ametangaza kwamba ameliomba Baraza la usalama wa taifa kuvifuta. Shughuli zao zimesitishwa kote nchini kwa kujiunga na rais wa zamani Joseph Kabila kupitia jukwaa lake la “Save the DRC”, lililoundwa katikati ya mwezi Oktoba jijini Nairobi, Kenya.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Kinshasa, Pascal Mulegwa
Kinshasa imeshutumu mkutano huu kama “wimbi jeusi” na Kabila, ambaye yuko chini ya hukumu ya kifo kwa madai ya ufadhili wake wa uasi wa AFC/M23.
Serikali ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo imetangaza kusitishwa kwa vyama vyote vilivyoshiriki katika mkutano wa Nairobi nchini Kenya, ulioitishwa na rais wa zamani Joseph.Kabila, ambao ulizindua jukwaa jipya la “Save the DRC“. Hadi sasa, ni vyama vitatu tu kati ya hivi, ikiwa ni pamoja na PPRD ya mkuu wa zamani wa nchi, vilivyokuwa vimesitishwa kwa jina la usalama wa taifa.
Ingawa haukuathiriwa moja kwa moja na hatu hii ya kusitishwa kwa vyama ya upinzani, muungano wa Lamuka, ulioundwa karibu na Martin Fayulu, unaushutumu kama “kikwazo kisichozeleweka kinachopinga demokrasia.” “Tunaomba Wizara ya Mambo ya Ndani kurejelea uamuzi wake. Tunahitaji mshikamano, umoja, na mazungumzo yanayoendelea,” amesema Prince Epenge, msemaji wa muungano huo. “Njia hii ya kusitiisha shughuli za vyama vilivyosajiliwa inatukumbusha enzi za utawala wa Kabila, ambao tulipambana tukiwa pamoja na UDPS.” Lakini kwa bahati mbaya, UDPS imeanza kuiga maadili hasi ya enzi ya Kabila.”
Vyama vinaandaa majibu yao
Wakati huo huo, serikali tayari imeomba Baraza la usalama wa kitaifa kufuta vyama hivi. Vita hivyo vitakuwa vya kisheria kwa upande wa chama cha LGD cha Matata Ponyo. “Bado ni adhabu kali,” anasema katibu mkuu wa chama hicho, Franklin Tshiamala. “Kwanza tutawasilisha rufaa yetu ya kiutawala ili kushughulikia sababu zisizo na msingi kuhusu adhabu hiyo. Na ikiwa hatajibu, tutawasilisha rufaa ya kisheria. Pia tutawasilisha rufaa yetu ya kimahakama kwa Baraza lile lile la usalama wa kitaifa ambalo aliomba kutufukuza au kutufuta, pia tutawasilisha sababu zisizo na msingi anazotoa.”
Mwanachama wa upinzani Delly Sessanga wa chama cha Envol, ambaye shughuli za chama chake hazikusitishwa, ameshtumu na kutaja hatua hiyo kama “ya kikatili na isiyo na na msingi wowote” na “utawala wa kimabavu usiokubalika.”