
Tetemeko la ardhi lililotokea kaskazini mwa Afghanistan usiku wa Jumapili, Novemba 2, kuamkia Jumatatu, Novemba 3, 2025, limesababisha vifo vya watu wengi, Wizara ya Afya imetangaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Tetemeko la ardhi lenye uzani wa 6.3 kwenye vipimo vya richter limeipiga Afghanistan usiku wa kuamkia leo na kusababisha vifo vya watu 20 na kuwajeruhi wengine 320.
Katika majimbo ya Balkh na Samangan, “takriban raia 320 wamejeruhiwa na zaidi ya 20 wamefariki,” amesema Sharafat Zaman, msemaji wa Wizara ya Afya, katika video iliyoshirikiwa na waandishi wa habari, akibainisha kuwa hii ilikuwa ni idadi ya awali ya vifo.
Tetemeko hilo limepiga kina cha kilomita 28 ardhini na karibu na Mazar-e Sharif, mji ulio na karibu watu 523,000.
Shirika la kitaifa la usimamizi wa majanga huko Afghanistan limesema litatoa taarifa kuhusiana na vifo au hasara zitatolewa baadae