
Tume ya Ulaya inatoa euro Milioni 9 kama msaada mpya wa kibinadamu kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) ili kushughulikia mahitaji ya kibinadamu ya kutisha yanayoikabili nchi hiyo. Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumatatu, Novemba 3, EU imebainisha kuwa ahadi hii ilitolewa wakati Kaja Kallas, Mwakilishi Mkuu wa Muungano wa Mambo ya Nje na Sera ya Usalama, alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Paris wa Amani na Ustawi katika Eneo la Maziwa Makuu.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Kulingana na taarifa hiyo, migogoro mashariki mwa DRC imezidisha kwa kiasi kikubwa mgogoro wa kibinadamu katika eneo hilo. Kuhama kwa watu wengi kumesababisha ongezeko la hitaji la vifaa muhimu kama vile chakula, maji, na malazi, pamoja na hatari kubwa kwa ulinzi wa makundi ambayo tayari yapo katika hatari kama vile wanawake na watoto.
Ufadhili wa euro Milioni 9 unakuja kujiongeza kwenye euro MiLioni 120 kama msaada wa kibinadamu ambao ulitolewa kwa eneo la Maziwa Makuu mwaka wa 2025. Eneo la mashariki mwa DRC ndilo kipaumbele.
Hadja Lahbib, Kamishna wa Maandalizi, Usimamizi wa Migogoro na Usawa, amesema:
“Mgogoro wa kibinadamu nchini DRC ni mojawapo ya matatizo makubwa zaidi ya wakati wetu. Kiwango cha mateso ya kibinadamu ni kikubwa na kinastahili kuzingatiwa kikamilifu. Kwa ufadhili huu mpya wa kibinadamu, EU inalenga kusaidia jamii zilizo katika mazingira magumu zaidi nchini DRC.”
EU inaendelea kujitolea, amebainisha, si tu kama mtendaji wa kibinadamu, bali pia kama mtetezi wa amani ya kudumu kwa raia wa Kongo.