Rais wa Mexico Claudia Sheinbaum amekataa uwezekano wa Marekani kuingilia kijeshi nchini Mexico siku ya Jumanne, Novemba 4, kufuatia ripoti za vyombo vya habari kwamba mwenzake wa Marekani, Donald Trump, alikuwa akifikiria kutuma wanajeshi kupambana na magenge yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya nchini Mexico.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Hilo halitatokea,” kiongozi huyo wa mrengo wa kushoto amesema alipoulizwa kuhusu ripoti hizo katika mkutano na waandishi wa habari. “Hatukubaliani” na uingiliaji wowote, ameongeza.

Trump aliishutumu Mexico kwa kutofanya vya kutosha kuzuia mtiririko wa dawa za kulevya nchini Marekani.

Mbali na kuyataja makundi kadhaa yanayofaya biashara ya madawa ya kulevya nchini Mexico kama makundi ya “kigaidi”, alipendekeza kupeleka wanajeshi Mexico kupambana na makundi hayo yanayofanya biashara ya madawa ya kulevya, pendekezo ambalo Bi. Sheinbaum alifutilia mbali hapo awali.

Wakati wa mkutano na Bi. Sheinbaum mnamo mwezi Septemba, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani Marco Rubio alisifu juhudi zake dhidi ya makundi yanayofanya biashara haramu ya madawa ya kulevya na kuahidi kwamba Marekani itaheshimu uhuru wa Mexico.

Lakini siku ya Jumatatu, NBC News iliripoti kwamba utawala wa Trump umeanza kuwafunza wanajeshi na maafisa wa ujasusi kwa ajili ya misheni inayowezekana katika ardhi ya Mexico, akiwataja maafisa wa sasa na wa zamani wa Marekani kwa sharti la kutotajwa jina. Hata hivyo hakuna uamuzi wa mwisho uliofanywa, kulingana na kituo hiki.

Operesheni ya Marekani katika ardhi ya Mexico itaashiria kuongezeka kwa kampeni ya kijeshi ya Donald Trump dhidi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya wa Amerika Kusini.

Mashambulizi ya Marekani dhidi ya meli zinazoshukiwa kuwa zinasafirisha madawa ya kulevya katika Pasifiki na Karibea katika wiki za hivi karibuni yaliua watu wasiopungua 65. Hadi sasa, mashambulizi mengi yamelenga meli za Venezuela.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *