Mfuko wa Watoto wa Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, hali ya maisha kwa watoto katika Ukanda wa Gaza ni mbaya mno.

Msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina amesema: “Hali ya maisha ya watoto katika Ukanda wa Gaza ni mbaya kutokana na hali ya hewa ya baridi, mvua kubwa na mafuriko.”

Kazem Abu Khalaf, msemaji wa Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF) huko Palestina amesisitiza kuwa: “Kiasi cha mahitaji katika Ukanda wa Gaza ni kikubwa sana, na tumesambaza mablanketi 600,000 na mahema 7,000 huko Gaza, lakini kiasi hicho hakikidhi mahitaji.”

Msemaji wa UNICEF pia amesema: “Mvua ni kubwa sana na maji yanaingia kwenye mahema.” Hapo awali, likiashiria dhoruba na mvua zinazoendelea kunyesha katika Ukanda wa Gaza, Shirika la UNICEF lilionya kwamba maisha ya zaidi ya watu 800,000 katika Ukanda wa Gaza yako hatarini, nusu yao wakiwa watoto.

UNICEF imekosoa utendaji wa jamii ya kimataifa katika Ukanda wa Gaza na kuongeza: “dunia imeshindwa na tumewaangusha watoto wa Gaza ambao wanaendelea kufa kutokana na sababu zinazoweza kuzuilika wakati wa majira ya baridi.” Takwimu zinaonyesha kuwa, watoto 82 wamefariki katika Ukanda wa Gaza tangu usitishaji vita uanze kutekelezwa, jambo ambalo linashangaza na lazima likomeshwe.

Wakati huo huo, imeelezwa kuwa, mvua kubwa zinazoendelea kunyesha huko Gaza hadi hivi sasa zimeshaharibu asilimia 90 ya mahema ya wakimbizi wa ukanda huo tena wakati huu wa kukaribia kuingia kwenye msimu wa baridi kali.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *