Michuano ya Kombe la Mataifa ya Afrika 2025 imeanza kutimua vumbii huko Moroko ikiwa ni mara yake ya 35 na ya kwanza kufanyika katika kipindi cha Krismasi na Mwaka Mpya.
DR Congo ni miongoni mwa timu zilizoshiriki mara nyingi ikiwa tayari imeshiriki mara ya 20 kwenye mashindano hayo, na ni moja ya timu zilizofanikiwa barani Afrika kwa kushinda taji hilo mara mbili, mnamo 1968 ikijulikana kama Kongo-Kinshasa, na 1974 kama Zaire.
Vijana wa Sebadtien Desabre wataanza kukipiga na Benin kesho kabla ya kucheza na Senegal.
Wakongomani wanaamini mwaka huu watafanya vyema kuliko mashindano yaliyopita.
David “Tutamtandika Benin ili tuanze vizuri na ili tupate matumaini ya kuanza kujitafutia tiketi ya 16 Bora, na kwenye hili kundi ambaye anaweza kuwa mwiba kidogo ni mtani wetu Senegal ambaye tuna kisasi naye”
Ramazani ” ukiangalia kile ambacho DRC walikifanya kwenye mchezo dhidi ya Nigeria na kwenye mchezo dhidi ya Cameroon ni kitu ambacho kimewashangaza wengi sana na nina imani kubwa sana Kongo atapita au kushinda kombe hili la Afcon 2025″
Moise Katumbi “tutafuzu, Wakati huu Kongo itaifungwa Senegali”
Leopards mara kadhaa wamekuwa na bahati ya kipekee kwenye kandanda haswa uwezo wao wa kubadilisha vipindi vya tabu kuwa mafanikio.