Ndegeza Marekani zimekuwa zikipataa katika maeneo mengi ya Nigeria kwa lengo la kukusanya taarifa za kijasusi tangu mwishoni mwa mwezi Novemba mwaka huu.

Harakati hizo za ndege za Marekani zinashuhudiwa katika maeneo mengi ya Nigeria kufuatia vitisho vya Rais Donald Trump mwezi Novemba mwaka huu vya kuingilia kijeshi nchini humo kuhusu kile alichodai kushindwa nchi hiyo kukomesha mateso ya Wakrito. 

Data ya ufuatiliaji ya mwezi huu wa Disemba inaonyesha kuwa ndege inayoendeshwa na wakandarasi wa Marekani na kutumika kwa shughuli za uchunguzi zimekuwa zikipaa kutokea Ghana na kuelekea Nigeria kabla ya kurejea Accra, mji mkuu wa Ghana. 

Wakati huo huo data ya  ufuatiliaji wa safari za ndege inaonyesha kuwa opareta wa safari hizo za ndege za kukusanya taarifa za ujasusi ni Tenax Aerospace yenye makao yake Mississippi na inafanya kazi kwa karibu na jeshi la Marekani.

Liam Karr, Mkuu wa Timu ya Africa Team Lead for the Threats Project at the American Enterprise Insitute amechambua data hizo za safari za ndege za Marekani. akisema operesheni hiyo ni ishara ya mapema kwamba Washington inajenga upya uwezo wake katika eneo la magharibi mwa Afrika baada ya Niger mwaka jana kuamuru kuondoka wanajeshi wa Marekani katika kambi kubwa ya anga iliyojengwa hivi karibuni nchini humo.

“Katika wiki za hivi karibuni tumeshuhudia kuanza tena safari za ndege za kijasusi na za uchunguzi za Mareani nchini Nigeria,” amesema Karr.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *