
Taifa ya Stars ya Tanzania ilishindwa kutamba mbele ya Nigeria na kukubali kichapo cha shingo upande cha magoli 2-1.
Uganda The Cranes wenyewe walijikuta kwenye hali mbaya zaidi kwa kubamizwa goli 3-1 walipokwaana na Tunisia mjini Rabat.
Hata hivyo, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo imewapa matumaini ya awali mashabiki wa soka wa Afrika Mashariki na Kati kwa ushindi wa kupapatua wa bao 1-0 mbele ya Benin.
Kwenye mechi nyingine, timu ya taifa ya Senegal au Simba wa Teranga, walikunjua makucha na kuwararua bao 3-0 vijana wa Botswana.
Hii leo mechi za ufunguzi wa hatua ya makundi zinamalizika kwa michezo minne ikiwemo itayaowakutanisha Ivory Coast dhidi ya Msumbiji na Algeria itakuwa na miadi na Sudan.