
Akizungumza na waandishi wa habari Zelensky amesema wanatarajia majibu kutoka kwa Urusi mara baada ya Marekani kuzungumza nao.
Akizungumzia maelezo ya mpango mpya wa vipengele 20 uliokamilishwa katika mazungumzo ya mwishoni mwa wiki huko Miami.
Rais Zelensky amesema kuwa rasimu ya pendekezo la kumaliza uvamizi wa Urusi ilipendekeza kwamba Ukraine, Urusi na Marekani ziendeshe kwa pamoja kinu cha nyuklia cha Zaporizhzhia kinachokaliwa na Urusi, hatua ambayo Kyiv inapinga.
Aidha Zelensky amesema Ukraine itaandaa uchaguzi wa rais haraka iwezekanavyo baada ya kusaini makubaliano ya kumaliza uvamizi wa Urusi.