Kupitia matandao wa X naibu Waziri wa Mambo ya Nje Sarah Rogers ameandika kwamba marufuku hiyo inawahusu Anna-Lena von Hodenberg na Josephine Ballon wakurugenzi wawili wakuu wa shirika la Ujerumani la HateAid, ambalo hupambana na unyanyasaji mtandaoni.

Shirika la HateAid, lililoanzishwa mwaka 2018, linachukuliwa kuwa kituo cha kwanza cha ushauri nchini Ujerumani kwa watu wanaokumbwa na unyanyasaji mtandaoni.

Marufuku hiyo pia imemlenga Thierry Breton, kamishna wa zamani wa Umoja wa Ulaya kutoka Ufaransa, ambaye anachukuliwa kuwa mmoja wa wabunifu wa Sheria ya Huduma za Kidijitali ya Umoja wa Ulaya, sheria inayodhibiti majukwaa ya mtandaoni.

Watu wengine wawili waliotajwa na Wizara ya Mambo ya Nje ni Imran Ahmed, mwanzilishi wa Center for Countering Digital Hate (US/UK), na Clare Melford, mwanzilishi wa Global Disinformation Index yenye makao Uingereza. Mashirika yote mawili hufanya kazi kupambana na kauli za chuki na upotoshaji mtandaoni.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *