
Nchini Kenya, mashirika ya kiraia yanatoa tahadhari kuhusu kuimarishwa kwa hatua za usalama wakati wa vipindi vya uchaguzi katika eneo hilo, Baada ya ukandamizaji mkali dhidi ya maandamano wakati wa uchaguzi nchini Tanzania mwishoni mwa mwezi Oktoba, ukandamizaji wa kisiasa nchini Uganda unatia wasiwasi wiki tatu kabla ya uchaguzi wa urais mnamo Januari 15.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Na mwandishi wetu huko Nairobi, Albane Thirouard
Mwanzoni mwa mwezi, Umoja wa Mataifa ulihesabu wapinzani 300 wa kisiasa waliokamatwa tangu kuanza kwa kampeni za uchaguzi mnamo mwezi Septemba. Mashirika yasiyo ya kiserikali yanalaani kurudi nyuma kwa demokrasia katika eneo hilo.
Ni kwa mshikamano na majirani zao watetezi wa haki za binadamu wa Kenya wamezungumza. Wanamdhtumu Rais wa Uganda Yoweri Museveni kwa kukiuka kimfumo haki za kisiasa za raia.
“Mashirika ya usalama yanaratibu kukandamiza kwa nguvu shughuli za upinzani, kutawanya mikusanyiko, kuwakamata viongozi wa upinzani na wafuasi wao wasio na hatia, na kuwatisha jamii. Uwepo wa vikosi vya kijeshi katika michakato ya kisiasa ya kiraia umeharibu dai lolote la ushiriki huru wa kisiasa,” analaani Geoffrey Mboya, mmoja wa wawakilishi wao.
Matumizi ya “mbinu za ukandamizaji”
Uganda imeweka vikwazo kwenye uingizaji wa vifaa vya Starlink, ambavyo sasa vinahitaji idhini kutoka kwa mkuu wa jeshi na mtoto wa Rais Museveni. Hili linamtia wasiwasi Mwanase Ahmed, mtetezi wa haki za binadamu nchini Kenya. “Hatu inayozuia uingizaji wa vifaa vya Starlink ni ishara ya kutisha sana. Kuna ishara nyingi ambazo zinaonyesha kuwa intaneti inaweza kufungwa wakati wowote; hii tayari ilitokea wakati wa uchaguzi uliopita wa urais mwaka wa 2021. Swali ni lini. Na pia nini kitatokea nyuma ya milango iliyofungwa,” anaongeza.
Mapema mwezi huu, Kamishna Mkuu wa Haki za Binadamu wa Umoja wa Mataifa alitoa wito kwa mamlaka ya Uganda “kuacha kutumia mbinu za ukandamizaji.” Alilaani haswa watu kukamatwa na kuwekwa kizuizini kiholela, pamoja na matumizi yasiyo ya kawaida ya nguvu dhidi ya upinzani.