
Wapiganaji wa RSF waliweka video kwenye mtandao wa kijamii ambazo zinaonesha wao kuwepo kwenye maeneo hayo.
Hakukuwa na taarifa yoyote kutoka kwa jeshi la Sudan kuhusu madai hayo.
Kati ya majimbo 18 ya Sudan, RSF inadhibiti majimbo matano ya eneo la Darfur magharibi mwa nchi, isipokuwa maeneo fulani ya Darfur Kaskazini ambayo bado yanadhibitiwa na jeshi.
Vita vimewaua maelfu ya watu
Jeshi, linadhibiti maeneo mengine ya majimbo 13 kusini, kaskazini, mashariki, na kati, ikiwemo mji mkuu wa Khartoum.
Mapigano hayo kati ya jeshi la Sudan na RSF, yaliyoanza Aprili 2023, yameua maelfu ya watu tangu wakati huo na kusababisha mamilioni wengi kukimbia makazi yao.