
Shamrashamra za Krismasi zinaendelea kote duniani leo Jumatano, siku ambayo Wakiristo wanasherehekea sikukuu ya kuzaliwa kwa Mwokozi wao Yesu Kristo wakati dunia ikielekeza macho yake katika vita vinavyoendelea kati ya Israel na kundi la wanamgambo la Hamas kutoka Palestina, katika Ukanda wa Gaza na maeneo mengine ya Palestina na Syria.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Wakristo duniani husherehekea Krismasi, sikukuu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Yesu Kristo, tarehe 25 Desemba (au Januari 7 kwa baadhi ya Orthodox), kwa njia mbalimbali kama ibada, mapambo, zawadi, na sherehe za familia, ingawa si Biblia inasema tarehe halisi, na awali haikuadhimishwa kila mwaka; hivi sasa ni sikukuu kubwa ya dunia inayochanganya imani na utamaduni, huku viongozi wa dini wakiitaka kuwa siku ya amani.
Mamia ya watu walikusanyika katika kanisa la Uzawa katika mji mtakatifu kwa Wakristo wa Bethlehem Jumanne kuadhimisha Krismasi nyingine iliyogubikwa na vita katika Ukanda wa Gaza.
Wakristo duniani kote wanamiminika Makanisani hii leo kuadhimisha siku kuu ya Krismasi. Kulingana na imani ya Kikristo, Krismasi ni siku kuu ambayo wanaamini kuwa Yesu Kristo (Isa) alizaliwa bethlehemu nchini israeli. Wakiristo wanaamini kuwa kuzaliwa kwa Yesu Kristo kuliwaletea ukombozi.
Tarehe 25 mwezi Desemba kila mwaka, Wakiristo kote duniani hutumia siku hiyo kwenda Makanisani na baadaye kusherehekea pamoja nyumbani na maeneo mengine kwa kula vyakula na kutoa zawadi.