Baada ya siku kadhaa za uhesabuji na uchunguzi wa kura huku kukiwa na mvutano, tuhuma za udanganyifu, na uingiliaji kati wa Donald Trump, mshindi wa uchaguzi wa rais nchini Honduras sasa anajulikana. Nasry Asfura, mgombea “kipenzi” wa rais wa Marekani na mhafidhina wa mrengo wa kulia, ameshinda uchaguzi uliofanyika Novemba 30.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Hatimaye Honduras inamjua mshindi wa uchaguzi wa rais uliofanyika Novemba 30. Tume ya Kitaifa ya Uchaguzi ilitangaza matokeo Jumatano, Desemba 24: mhafidhina Nasry Asfura ameshinda kwa 40.3% ya kura dhidi ya 39.5% aliyepata mpinzani wake, mrengo wa kati Salvador Nasralla. Wiki kadhaa za kusubiri, matokeo yanayokaribiana, na hesabu zenye utata, huku 15% ya karatasi za kuhesabu kura zikipaswa kuchunguzwa kwa mikono.

Baada ya miaka minne ya utawala wa Rais Xiomara Castro wa mrengo wa kushoto, ushindi huu unasisitiza kuibuka kwa serikali za mrengo wa kulia Amerika Kusini kufuatia mabadiliko ya madaraka nchini Chile, Bolivia, Peru, na Argentina. Hata hivyo, nchi hizi zenye uchumi kubwa zaidi katika eneo hilo, Brazili na Mexico, zinendelea kutawaliwa na vyama vya mrengo wa kushoto.

Tuhuma za ubadhirifu

Mshindi, Nasry Asfura, ana umri wa miaka 67. Mtoto wa wahamiaji wa Palestina, kutoka Chama cha National Party, chama kilichochukua madaraka baada ya jaribio la mapinduzi la mwaka 2009.

Miongoni mwa mafanikio yake, Nasry Asfura ana vipindi viwili vyenye utata kama meya wa mji mkuu wa nchi hiyo, ambapo anatuhumiwa kwa ubadhirifu wa zaidi ya euro milioni 7 kwa kampuni yake ya ujenzi. Jina lake pia lilionekana katika “Panama Papers.”

Akiungwa mkono katika kampeni yake yote na Donald Trump, ushindi wake ulipongezwa mara moja na Marco Rubio, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, ambaye amekiri ushindi wa “wazi” na “usiopingika”, akitoa wito kwa pande zote “kuheshimu matokeo.”

“Tunatarajia kufanya kazi na utawala wake ili kuendeleza ushirikiano wetu wa usalama wa pande mbili na kikanda, kukomesha uhamiaji haramu nchini Marekani, na kuimarisha uhusiano wa kiuchumi kati ya nchi zetu mbili,” ameongeza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *