
Watu watano walifariki katika ajali ya helikopta kwenye Mlima Kilimanjaro, mlima mkuwa zaidi barani Afrika, nchini Tanzania, mamlaka zimetangaza.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Ajali hiyo ilitokea siku ya Jumatano jioni katika moja ya njia maarufu za watalii, wakati wa misheni ya uokoaji kuwasaidia wagonjwa mlimani, kulingana na polisi.
Wageni wawili, ambao, kulingana na polisi, walikuwa wamehamishwa kwa sababu za kimatibabu, walikuwa miongoni mwa waathiriwa.
Daktari wa eneo hilo, mwongozo wa watalii, na rubani pia walifariki katika ajali hiyo.
Kulingana na vyombo vya habari vya Tanzania, raia wa Jamhuri ya Czech na Mzimbabwe walikuwa ndani ya helikopta hiyo.
Ajali hiyo ilitokea kati ya Kambi ya Barafu na kilele cha Kibo, katika mwinuko wa zaidi ya mita 4,000.
Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kilimanjaro Simon Maigwa amewaambia waandishi wa habari kwamba ndege hiyo ilikuwa ya kampuni ya uokoaji Kilimanjaro Aviation, ambayo bado haijatoa maoni kuhusu ajali hiyo.
Kwa mujibu wa taarifa rasmi, waliopoteza maisha ni Plos David na Plosova Anna raia wa Jamuhuri ya Czech walipandishwa mlimani kutalii na kampuni ya Mikaya Tours, Jimmy Daniel (daktari), Innocent Mbaga ambaye alikuwa muongoza watalii na rubani Costantine Mazonde raia wa Zimbabwe.
Siku ya Alhamisi Mamlaka ya Usafiri wa Anga ya Tanzania ilitangaza kwamba imeanzisha uchunguzi, kwa mujibu wa viwango vya usalama vya kimataifa, “ili kubaini mazingira na chanzo kinachowezekana” cha ajali hiyo.
Ajali za ndege Kilimanjaro ni nadra. Tukio la mwisho lililorekodiwa lilitokea Novemba 2008 na kusababisha vifo vinne.
Kilimanjaro huvutia maelfu ya watalii kila mwaka. Ingawa kupanda huko hakuleti matatizo makubwa ya kiufundi, mwinuko ni tatizo kwa wapandaji wengi.