Urusi yashambulia miundombinu ya umeme KyivUrusi yashambulia miundombinu ya umeme Kyiv

Meya wa Kyiv, Vitaliy Klitschko, amesema watu 19 wameathirika kufutia shambulio hilo, 11 kati yao wamelazwa hospitalini.

Miundombinu ya umeme na gesi inayowezesha joto la ndani wakati wa baridi imeharibikia, na kuathiri zaidi ya majengo 2,600 ya makaazi pamoja na mamia ya shule na taasisi za kijamii.

Shambulio hilo limetokea siku moja kabla ya Rais Volodymyr Zelensky kukutana na Rais wa Marekani Donald Trump mjini Florida kujadili mpango wa kuvimaliza vita vilivyoanza mwaka 2022.

Urusi imemtuhumu Zelensky na washirika wake wa Umoja wa Ulaya kwa kile ilichotaja kama kutaka “kuuharibu” mpango huo unaosimamiwa na Marekani.

Kulingana na maelezo yaliyotolewa na Zelensky mapema wiki hii, mpango huo mpya una vipengele 20 vinavyopendekeza kusimamisha vita na kuanzisha maeneo yasiyo na jeshi mashariki mwa Ukraine.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *