
Kwa mujibu wa waendesha mashtaka wa kupambana na ugaidi nchini Italia, watuhumiwa wanadaiwa kutuma takriban euro milioni 7 kwa “mashirika yaliyo na makaazi Gaza, maeneo ya mamlaka ya Palestina, Israel au maeneo yanayohusishwa na udhibiti wa Hamas.”
Waendesha mashtaka wamesema fedha hizo haramu zilipitishwa kupitia “mzunguko wa taasisi kadhaa” kwa njia ya uhamisho wa benki au kupitia mashirika yaliyo nje ya nchi kwenda Gaza na ambayo Israel imeyatangaza kuwa haramu kutokana na uhusiano wao na Hamas. Uchunguzi huo ulihusisha ushirikiano na nchi nyingine za Umoja wa Ulaya.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Italia, Matteo Piantedosi, ameandika kupitia mtandao wa kijamii wa X kwamba operesheni hiyo imefichua shughuli zilizodai kuwasaidia Wapalestina ilhali zinaunga mkono mashirika ya kigaidi.