Katika kundi D, muda mfupi uliopita Benin imeibuka na ushindi mwembamba ya 1-0 dhidi ya Botswana. Bao la pekee likitiwa kimyani na Yohan Roche kunano dakika ya 28 ya mchezo.

Hapo baadaye Senegal itaingia uwanjani kucheza dhidi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo alafu kuanzia saa mbili unusu majira ya Afrika Mashariki, wakati majirani wa Afrika Mashariki – Uganda na Tanzania watapambana katika uwanja wa Al Medina mjini Rabat.

Super Eagles ya Nigeria iliyopata ushindi wa mabao 2-1 katika mechi yake ya kwanza dhidi ya Tanzania, itakabiliana na Tunisia.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *