Wapiga kura milioni 6.7 wa Guinea wanapiga Jumapili hii, Desemba 28, kwa ajili ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais. Uchaguzi huu, ambao utaashiria kurudi kwa utaratibu wa kikatiba baada ya zaidi ya miaka minne ya mpito. Wagombea wanane akiwemo Abdoulaye Yéro Baldé na Faya Millimouno wanawania katika kinayang’anyiro hiki cha urais dhidi ya rais wa mpito, Mamadi Doumbouya.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu huko Conakry, Tangi Bihan

Kwa kumpindua Alpha Condé, Mamadi Doumbouya aliahidi kutogombea katika uchaguzi wa urais wa Guinea. Lakini hapa yuko, kwenye mstari wa kuanzia, ili kuimarisha mafanikio ya mpito na kuendeleza maendeleo ya kiuchumi ya nchi, kulingana na Waziri Mkuu wake, Bah Oury. Akiwa mgombea asiye na wasiwasi, kuonekana kwake katika kampeni za uchaguzi kulipunguzwa kwa video na hotuba zilizorekodiwa awali. Aliwaachia nafasi mawaziri wake kutetea rekodi yake na mpango wake kwa wapiga kura waliokuwa wakija kuhudhiria kampeni za chama chake.

Abdoulaye Yéro Baldé, waziri huyu wa zamani wa Elimu ya Juu aliyejiuzulu katika serikali ya Alpha Condé akipinga azma yake ya kuwania muhula wa tatu, naye pia anawania katika uchaguzi huu. Kiongozi mwingine ambaye alikuwa mkosoaji, Faya Millimouno wa Kambi ya Kiliberali, amekuwa akishutumu mara kwa mara kutoweka kwa watu mashuhuri wa upinzani na kufungwa kwa vyombo vikuu vya habari katika kipindi chote cha mpito pia anawania katika uchaguzi huu. Pia wagombea wengine katika kinyang’anyiro hiki ni mwanadiplomasia wa zamani na Waziri wa Mambo ya Nje Makalé Camara, mgombea pekee mwanamke, na Mohamed Nabé wa Muungano wa Ufufuaji na Maendeleo.

Hatimaye, uchaguzi huu unaoshuhudiwa na kutokuwepo kwa watu mashuhuri ambao wameunda maisha ya kisiasa ya Guinea katika kipindi cha miaka thelathini iliyopita, kama vile Alpha Condé, Cellou Dalein Diallo, na Sidya Touré, ambao wote wako uhamishoni. Vyama vyao vinawataka wanachama wao kubaki nyumbani. Wagombea wengine katika uchaguzi huu ni Bouna Keita, Abdoulaye Kourouma, Mohamed Chérif Tounkara, na Ibrahima Abé Sylla.

Uchaguzi chini ya uangalizi wa waangalizi kadhaa

Waangalizi kutoka mashirika kadhaa ya kimataifa kama vile Umoja wa Afrika, ECOWAS, na Umoja wa Ulaya wako nchini Guinea kwa uchaguzi huu. Lakini pia na waangalizi wa kitaifa, ambao tayari wametumwa. Wanatarajia uchaguzi wa amani, ingawa wananyooshea kidole hatari fulani.

Miongoni mwa mashirika ya kiraia yanayotuma waangalizi ni Mtandao wa Kujenga Amani wa Afrika Magharibi (WANEP), ambao unaa hofia ya kutokea hatari za vurugu. Kulingana na mkurugenzi wake, Tamba Jean Tolno, ingawa kampeni imekuwa ya amani, kutokuwepo kwa vyama vikuuu vya siasa na wito wao wa kususia kuna hatari ya kutokea vurugu.

“Viongozi wamewataka wafuasi wao kukaa nyumbani na kutoshiriki katika uchaguzi huu. Watu wanaweza kufikiria kwamba kususia kunamaanisha kuwazuia wale wanaotaka kupiga kura kwenda kupiga kura. Na hilo linaweza kusababisha vurugu.” “Hiyo ndiyo hatari kuu tunayohofia wakati wa uchaguzi huu.”

Hata hivyo, amebainisha uhakikisho kuhusu hatua za usalama zinazotumiwa na mamlaka. Miongoni mwa waangalizi wengine ni chama cha Wanablogu wa Guinea (Ablogui), ambacho kimebobea katika masuala ya kidijitali. Ingawa ufikiaji wa Facebook umezuiwa tangu siku ya Jumatatu, Desemba 22, kiongozi wake, Baro Condé, anahofia vikwazo vipana zaidi, kama ilivyokuwa wakati wa kura ya maoni ya mwezi Septemba, ambavyo vinaweza kuzuia kazi yao.

Mashirika haya yatawasilisha ripoti zao za kwanza mnamo Desemba 28.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *