
Israel kuitambuwa Somaliland, ambayo “inahimiza” harakati za kujitenga duniani kote, ni “tishio” kwa usalama na utulivu wa Pembe ya Afrika, Rais wa Somalia Hassan Sheikh Mohamud ametangaza mnamo Desemba 28, 2025.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
“Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amefanya ukiukaji mkubwa zaidi wa uhuru wa Somalia,” Sheikh Mohamud ameyaambia mabunge yote mawili (Baraza la Bunge na Baraza la Seneti) ya Somalia, ambayo yameitishwa katika kikao cha kipekee kutokana na mgogoro unaoikumba nchi hiyo.
Aeongeza kuwa Mogadishu “haitakubali kamwe” Israel kuwafukuza Wapalestina kutoka Gaza kwenda Somaliland , kama baadhi ya vyombo vya habari vilivyobainisha miezi michache iliyopita, madai ambayo mamlaka ya Somaliland wala serikali ya Israel hazikutoa maoni yoyote.
Israel inakuwa taifa pekee duniani linaloitambua Somaliland kama “taifa huru na linalojitawala,” utambuzi ambao ni “wa pande zote mbili,” kulingana na taarifa rasmi ya Israel.
Katika taarifa hii, Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu anarejelea “moyo wa Makubaliano ya Abraham,” akimaanisha wimbi la kuhalalisha ambalo lilishuhudia Falme za Kiarabu, Bahrain, Morocco, na Sudan zikianzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israel mwaka wa 2020. Sudan, ambayo tangu wakati huo imekuwa ikikumbwa na vita, haijaidhinisha kufufua uhusiano huu.
Kwa upande wa athari, kutambuliwa kwa Somaliland hakuhusiani sana na matarajio ya kufuua uhusiano na Saudi Arabia, ambayo kwa muda mrefu ilitarajiwa na Israeli lakini kwa sasa imezuiwa na Riyadh kutokana na sera ya taifa la Kiyahudi kwa Wapalestina.