Mabao ya Msumbiji yakitiwa kimyani na Faisal Bangal, Genny Camato na Diogo Calila.

Pierre- Emerick Aubameyang alijaribu kuirudisha mchezoni Gabon kwa kupachika bao kabla ya kipindi cha kwanza kukamilika, na Alex Moucketou- Moussounda kuongeza la pili lakini Gabon haikuweza kusawazisha.

Guinea ya Ikweta ikachuana na Sudan, Algeria ikutane na Burkina Faso na mechi inayosubiriwa kwa hamu ni kati ya Ivory Coast na Cameroon.

Kwengineko, Kocha wa Morocco Walid Regragui amethibitisha kuwa nahodha Achraf Hakimi yuko katika hali nzuri kucheza dhidi ya Zambia katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A kwenye Kombe la Mataifa ya Afrika siku ya Jumatatu, baada ya kukosa kuanza katika mechi mbili za awali za mashindano hayo.

Hakimi alitangazwa kuwa Mchezaji Bora wa Afrika katika tuzo za Shirikisho la Soka Afrika mwezi uliopita, lakini alihudhuria hafla hiyo mjini Rabat akiwa na magongo ya kutembele, jambo lililoibua mashaka iwapo angepona kwa wakati kabla ya fainali ya AFCON.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *