MSANII wa muziki wa kizazi kipya nchini, Rajab Abdul maarufu kama ‘Harmonize’, na mwigizaji Frida Kajala, wamevuta hisia za wadau wa burudani baada ya kuvishana pete ya uchumba kwa mara ya pili.

Hatua hiyo imekuja ikiwa ni takriban miaka mitatu tangu walipovishana pete mwaka 2022, kabla ya kutengana na kusitisha mpango wa kufunga ndoa, hali iliyozua maswali mengi kwa mashabiki.

Tukio la sasa limechukuliwa na wengi kama ishara ya dhamira ya dhati ya wawili hao kurejesha mahusiano yao na kufikia hatua ya ndoa. SOMA: Harmonize, Abigail wazindua Hit ya Kimataifa

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *