Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Dkt. Bashiru Ally, amesema Serikali ina mpango wa kupanua masoko ya nyama katika soko la kimataifa kwa kuuza tani 50,000 kwa mwaka, kutoka tani 14,000 zinazouzwa kwa sasa.
Waziri amesema hayo alipokuwa akizungumza na wadau wa sekta ya ufugaji wakati wa kuhitimisha ziara yake ya kikazi ya siku mbili mkoani Kagera. Amesema hatua hiyo inalenga kuongeza thamani ya mazao ya mifugo, kukuza uchumi wa wafugaji na kuongeza mapato ya Taifa kupitia mauzo ya nje.
✍Benson Eustace
Mhariri | @claud_jm
#AzamTVUpdates