“Watu kadhaa” wamefariki na kujeruhiwa katika baa iliyojaa watu katika hoteli ya kifahari nchini Uswisi ya Crans-Montana wakati moto ulipozuka huku wahudhuriaji wakisherehekea Mwaka Mpya, polisi imetangaza leo Alhamisi, Januari 1, 2026.

Imechapishwa:

Dakika 2 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Alhamisi, Januari 1, 2026, yapata saa 7:30 usiku saa za Uswisi (saa 7:30 saa za Ufaransa), “moto ambao haujabainika ulizuka katika baa ya Constellation huko Crans-Montana,” eneo maarufu kwa watalii, polisi wa jimbo la Valais kusini magharibi mwa Uswisi wamesema katika taarifa. “Watu kadhaa wamepoteza maisha na wengine wamejeruhiwa. Idadi kubwa ya wafanyakazi wa kitengo cha idara ya huduma za dharura” imetumwa katika eneo la tukio, polisi wameongeza, wakielezea tukio hilo kama “kubwa.”

“Idadi kubwa ya vifo na majeruhi”

“Idadi kubwa ya vikosi vya polisi, wazima moto, na vikosi vya uokoaji vimetumwa mara moja kwenye eneo la tukio ili kuwasaidia waathiriwa wengi,” vikosi vya usalama vimesema, vikiongeza kuwa operesheni “bado inaendelea.” Hakuna idadi rasmi ya vifo inayopatikana mara moja, lakini vyombo kadhaa vya habari vya Uswisi vinaripoti idadi kubwa ya majeruhi. Gazeti la kila siku la Blick, likimnukuu daktari aliyekuwepo, linabaini kwamba wafu wanaweza kuwa katika “dazeni.” Gazeti la kila siku la kikanda la Le Nouvelliste linaripoti kwamba vyanzo vyake vinaelezea “idadi kubwa,” huku “takriban 40 wakifariki na 100 wakijeruhiwa.”

Picha zilizorushwa na vyombo vya habari vya Uswisi zimeonyesha jengo lililoungua na watu wakikimbia na kupiga kelele gizani. Polisi wa Uswisi wanabaini kwamba chanzo cha moto bado hakijajulikana, lakini baadhi ya vyombo vya habari vinabaini kwamba moto huo unaweza kuwa ulisababishwa na vifaa vya pyrotechnic vilivyotumika wakati wa tamasha. Mapema alfajiri mpiga picha wa shirika la habari la AFP aliona magari mengi ya wagonjwa barabarani yanayoelekea kwenye kituo cha michezo ya kuteleza kwenye theluji ambako tukio hilo lilitokea.

Helikopta nyingi zatumwa

Kulingana na Gazeti la Uswisi 24 Heures, lililonukuliwa na shirikala habari la AFP, “helikopta zinaendelea na upekuzi wao karibu saa saba baada ya kuanza kwa mkasa huo.” Njia ya kufikia baa ilikuwa imefungwa, na yapata saa 2:00 asubuhi ya leo, “polisi wa uchunguzi walikuwa tayari wakifanya kazi ndani ya jengo hilo,” lililoko kwenye ghorofa ya chini, kulingana na gazeti hilo. Watu waliokuwa wakitafuta ndugu zao walielekezwa kwenye kituo cha mikutano ambapo operesheni ya upekuzi ilikuwa imeanzishwa. “Mwanangu hapatikani,” mama mmoja aliyekuwa akilia, aliyenukuliwa na Gazeti la 24 Heures, alisema, “hakuna anayejua alipo.”

Mkazi wa Crans-Montana pia ameliambia Gazeti la 24 Heures kwamba “kwa fataki, hatukuelewa kilichokuwa kikiendelea. Na kisha tukaona moshi.” Mkazi mwingine, anayeishi mita chache tu kutoka Constellation, amesema aliarifiwa kuhusu mkasa huo alipokuwa akisherehekea Mkesha wa Mwaka Mpya nyumbani na marafiki. “Nilishuka hadi barabarani,” barbara ambayo “tayari ilikuwa imefungwa na polisi. Tuliweza kusikia ving’ora vya taa zinazowaka kwa mbali. Karibu nami, watu walipigwa na butwaa, walikuwa na wasiwasi, na walikuwa kimya.”

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *