
Moto mkubwa umeteketeza kanisa la karne ya 19 huko Amsterdam siku ya Alhamisi, Januari 1, huku Uholanzi ikisheherekea mkesha wa Mwaka Mpya. Watu wawili wamefarik. Vifo hivyo vinahusishwa na fataki na vurugu ambazo hazikutarajiwa dhidi ya polisi.
Imechapishwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Mnara wa Kanisa la Vondel huko Amsterdam umeanguka kutokana na moto ulioteketeza jengo hilo usiku wa kuamkia Mwaka Mpya. Wazima moto walikuwa bado wakipambana na moto huo leo Alhamisi asubuhi. Mamlaka inasema kanisa hilo haliwezi kuokolewa.
Kanisa maarufu katika mji mkuu wa Uholanzi lilishika moto usiku wa kuamkia Mwaka Mpya. Kanisa la Vondel, moja ya alama muhimu za Amsterdam, liliteketea kwa moto, huku mnara ukianguka, na sehemu kubwa ya paa imeharibika.
Mnara huo wenye urefu wa mita 50 ulianguka na paa likaharibika vibaya, imesema mamlaka ya Amsterdam, kwa mujibu wa shirika la habari la AFP.
Moto huo ulizuka muda mfupi baada ya usiku wa manane. Moshi mkubwa ulionekana angani usiku juu ya mji mkuu wa Uholanzi, huku sherehe za Mwaka Mpya zikiendelea katikati ya jiji.
Asubuhi ya Alhamisi, Januari 1, wazima moto wa Uholanzi walikuwa bado wakifanya kazi ya kuzima moto huo. Hakuna majeruhi walioripotiwa, lakini watu walio maeneo jirani ya kanisa hilo wamehamishwa, kulingana na vyombo vya habari vya Uholanzi.
Kanisa “haliwezi kuokolewa”
Kulingana na maafisa wa usalama walionukuliwa na vyombo vya habari vya ndani, kanisa “haliwezi kuokolewa” na haliwezi kutengenezwa. Vondelkerk iko katika hatari ya kuanguka kabisa. Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana kufikia leo Alhamisi asubuhi.