
Marekani. Kwa mujibu wa nyota wa New England Patriots, Stefon Diggs, na mpenziwe rapa wa Marekani, Cardi B, wanatarajia kupata mtoto wa kiume muda wowote kuanzia sasa.
Uhusiano wa Cardi B na Diggs ulianza kama uvumi Oktoba 2024, ingawa Cardi B alikanusha mara kadhaa. Hata hivyo, mashabiki waligundua picha na video mbalimbali zilizowaonyesha wawili hao wakiwa pamoja na kuanza kushuku kuwa kulikuwa na uhusiano wa kimapenzi kati yao.
Diggs alithibitisha jinsia ya mtoto wao kwa People akiwa kwenye Tuzo za Mitindo za CFDA 2025, “Ni mvulana. Hiyo inanitosha.”
Akaongeza kuwa anafurahia kufundisha mwanawe michezo na mazoezi. “Siwezi kusubiri kumfanya afanye push-up, sit-up na kukimbia huku na kule,” Diggs alisema.
Aidha, katika mahojiano mengine Diggs alisema muda wa mama kujifungua umekaribia. “Inaweza kutokea muda wowote sasa kwa hiyo, tutakieni kheri ajifungue salama.”
Mwezi huo huo aliotangaza ujauzito Cardi aliachia albamu mpya Am I the Drama?, iliyoshika nafasi ya kwanza kwenye Billboard 200.Ujauzito wake haujakosa drama kwani mwanadada huyo aliingia mitaani na kuuza muziki mwenyewe.
Tetesi zilianza kushika kasi zaidi baada ya Cardi B kuachana rasmi na Offset, mumewe wa zamani.
Mnamo Mei 2025, uvumi huo ulithibitishwa wazi pale walipoonekana wakifurahia pamoja kwenye mchezo wa mpira wa kikapu huku Cardi akionekana akimkumbatia na kumbusu Diggs kwenye skrini kubwa ya ukumbi.
Miezi michache baadaye, wawili hao walitangaza uhusiano wao rasmi kupitia Instagram, jambo lililowashangaza mashabiki wengi kwani hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa Cardi kutangaza hadharani uhusiano mpya tangu alipotalikiana na Offset mwezi Julai 2024.
Cardi B na Offset walidumu kwenye ndoa yao kwa takribani miaka saba, walianza kuchumbiana mwaka 2017 na baadaye kufunga ndoa ya kimya Septemba mwaka huohuo.
Katika kipindi chote hicho walipata watoto watatu, hata hivyo, ndoa yao ilikumbwa na changamoto nyingi za misukosuko na mwaka 2024 wakaamua kuachana.
Chanzo cha kuvunjika kwa ndoa hiyo ilidaiwa kuwa tuhuma za usaliti, Offset mara kadhaa alihusishwa na kashfa za usaliti, ingawa Cardi B aliwahi kumsamehe, hali hii iliendelea kuleta mizozo ndani ya ndoa.
Rapa huyo na Diggs walijulikana hadharani wakati wa Siku ya Wapendanao mapema mwaka huu na Aprili walionekana pamoja kwenye tamasha la Coachella.
Walitangaza Septemba kwamba wanatarajia mtoto, ambapo Cardi aliambia kipindi cha CBS Mornings: “Nimefurahia nafanya kazi zote hizi huku nikiwa na mtoto tumboni, mimi na mwanaume wangu tunasaidiana sana.”