Uturuki siku ya Jumatatu imelaani shambulizi la ndege zisizo na rubani kwenye kambi ya Umoja wa Mataifa nchini Sudan na kuua walinda amani sita wa Bangladesh na kuwajeruhi wengine wanane.

“Tunawatakia rehema za Mwenyezi Mungu ziwafikie walinda amani wa Bangladesh waliopoteza maisha katika shambulio hili baya, na ahueni ya haraka kwa waliojeruhiwa,” Wizara ya Mambo ya Nje ya Uturuki ilisema katika taarifa.

Wizara hiyo ilisisitiza umuhimu wa kuhifadhi uhuru wa mipaka wa eneo la Sudan, na ikasisitiza “uungaji mkono mkubwa kwa juhudi zinazolenga kutafuta suluhu la amani kwa migogoro inayoendelea nchini humo.”

Shambulio hilo limetokea huku mzozo kati ya jeshi la Sudan na kikosi RSF ukiendelea bila ya kusitishwa. Mapigano yalionaza tangu Aprili 2023 yamesababisha vifo vya maelfu, mamilioni ya watu kuyahama makazi yao na kusababisha moja ya machafuko mabaya zaidi ya kibinadamu duniani.

Jeshi la Sudan lililaumu kikosi cha RSF. Hata hivyo hadi sasa hakuna ufafanuzi wowote kutoka kundi hilo la waasi.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *