
Mshtakiwa anakabiliwa na mashtaka mawili ya mauaji na mashtaka 44 ya kujaribu kuua kufuatia tukio hilo la Februari 13.
Waendesha mashtaka wanasema raia huyo wa Afghanistan “alichochewa na ari ya kidini iliyokithiri” alipofanya shambulio hilo.
Waendesha mashtaka wa serikali wanasema kwamba wakati wa kuhojiwa, mshtakiwa alizungumzia hisia ya wajibu wa kuwaua watu kiholela nchini Ujerumani kama jibu la moja kwa moja kwa mateso ya Waislamu duniani kote.
Shambulio hilo, ambalo liliyalenga maandamano yaliyofanyika wakati wa Mkutano wa Usalama wa Munich (MSC), lilimuua mwanamke mwenye umri wa miaka 37 na binti yake wa miaka 2, pamoja na kuwajeruhi vibaya watu wengine 44.
Farhad N. alikamatwa katika eneo la tukio hilo la kihalifu na amekuwa mikononi mwa polisi tangu wakati huo.
Mamlaka zinasema Farhad N. alinyimwa hifadhi nchini Ujerumani lakini zinasisitiza kwamba hata hivyo aliishi nchini humo kihalali.
Wanasema shambulio lake halikulenga mkutano wa usalama wa MSC — amba kila mwaka huwakusanya wanasiasa wa ngazi za juu wa kimataifa — bali maandamano ya chama cha wafanyakazi yaliyojaa watu. Kesi yake inatarajiwa kukamilika mwishoni mwa Juni 2026.