
Nigeria imeanza kutekeleza mfumo mpya wa kukusanya kodi, ambao serikali inasema, itaongeza kiwango cha kodi na kupunguza ugumu wa kiuchumi kwa raia wa kawaida, hasa wanaojihusisha na biashara ndogo ndogo.
Imechapishwa: Imehaririwa:
Dakika 1 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Hatua hii inakuja, baada ya kutiwa saini kwa sheria mpya kuhusu kodi mwezi Juni mwaka uliopita, licha ya upinzani kutoka kwa upinzani, wanaoishtumu serikali ya rais Bola Tinubu kwa kuanza kutekeleza utaratibu mpya wanaosema ni kinyume cha sheria.
Sheria hii mpya inaongeza kiwango cha kodi kinachokusanywa, hatua ambayo serikali inasema ni ahueni kwa raia wa Nigeria wenye kipato cha chini.
Katika ujumbe wake wa mwaka mpya, rais Tinubu alisistiza kuwa ni lazima, sheria hiyo mpya ianze kutekelewa kuanzia Januari tarehe 1, akisema hatua hiyo itasaidia kuimarisha uchumi wa taifa hilo la Afrika Magahribi.
Nigeria ambayo ina majimbo 36, yanayoongozwa na Magavana, kwa miaka mingi imekuwa ikipambana kuhusu namna ya kuzifanyia marekebisho sheria kuhusu ukusanyaji wa kodi, ili kuwe na mfumo sawa.