Nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati, wakati matokeo ya sehemu ya uchaguzi mkuu wa Desemba 28, 2025 yakianza kutangazwa, mapigano yamezuka kusini mashariki mwa nchi kati ya wanamgambo wa AAKG na vikosi vya serikali. Mji wa Zémio ulishambuliwa jioni ya Januari 1.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Afrika ya Kati, Buno Yapandé, hali kwa sasa imedhibitiwa, baada ya watu kadhaa wenye silaha wa kundi la Azandé Ani Kpi Gbé (AAKG) – kundi la kujilinda la jamii ya Zandé na mshirika wa zamani wa serikali ambalo sasa linapinga serikali ya Bangui – ​​lilishambulia kituo cha ukaguzi nje kidogo ya mji wa Zémio siku ya Alhamisi jioni, na kuwajeruhi baadhi ya wanajeshi wa Jamhur ya Afrika ya Kati (CAR), kabla ya Misheni ya Umoja wa Mataifa (MINUSCA) kuingilia kati kuwafukuza.

Mapigano yanaripotiwa kuanza tena Ijumaa asubuhi hii: mwanamke ameuawa, kulingana na mamlaka. Askari wa vikosi vy jeshi la Afrika ya Kati (FACA) pia anaripotiwa kufariki, lakini taarifa hii bado haijathibitishwa.

Takriban watu 2,500 wametafuta hifadhi Sudan Kusini.

Yote yalianza siku ya Jumapili ya wiki iliyopita wakati wanamgambo wa AAKG walipovuruga uchaguzi mkuu nchii Jamhuri ya Afrika ya Kati katika mji wa Bambouti, kwenye mpaka na Sudan Kusini, na kumteka nyara mkuu wa mkoa, polisi, na afisa wa uchaguzi ambaye tangu wakati huo aliuawa. Katika kulipiza kisasi, FACA na washirika wao wa Urusi walianzisha operesheni ya kijeshi katika mji huo, wakituma helikopta kadhaa.

Takriban watu 2,500 wamekimbia Bambouti na kutafuta hifadhi upande wa pili wa mpaka, kulingana na Umoja wa Mataifa. Asubuhi ya leo, mapigano yameendelea na shambulio jipya katika mji huo, kulingana na vyanzo kadhaa. Hata hivyo, utulivu umerejea, kulingana na Buno Yapandé. Lakini ukosefu wa mtandao wa simu unachanganya upatikanaji wa taarifa, huku mazungumzo yakiendelea ili kuweza kuachiliwa kwa mateka hao, kulingana na waziri.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *