
Akiandika katika mtandao wake wa Social Truth, Trump amesema anaihimiza Cuba kumsikiliza mapema kabla ya muda kufikia mwisho.
Kauli yake inakuja wiki moja baada ya vikosi vya Marekani kumkamata rais wa Venezuela Nicolas Maduro, katika operesheni ya kijeshi iliyofanyika Caracas iliyowaua wanajeshi wa Venezuela na wale wa Cuba waliokuwa huko kwa operesheni maalum ambayo bado haijafafanuliwa hadi sasa.
Awali Trump alituma ujumbe wake huko akiashiria kuwa Waziri wa mambo ya nje wa Marekani Marco Rubio, anaweza kuwa rais wa taifa hilo la kikomunisti la Cuba. Amesema Cuba ilitoa ulinzi kwa wadikteta wawili kwa Venezuela akisisitiza kwamba hilo halitowezekana tena.
Cuba imekuwa ikifaidika na mafuta ya Venezuela kufuatia makubaliano yaliyofanyika baina ya mataifa hayo mawili chini ya kiongozi wa zamani wa Caracas Hugo Chavez.