Ndani ya siku za mwanzo za vita vyake na wanamgambo wa RSF mwezi Aprili mwaka 2023, Serikali hiyo inayoungwa mkono na jeshi iliutoroka mji wa Khartoum, uliodhibitiwa wakati huo na makundi pinzani.

Imekuwa ikichukua hatua za kurejea mjini humo tangu jeshi lilipoudhibiti tena mji wa Khatoum, Sudan mwezi Machi mwaka jana.

Kamil Idris, aliyewaahidi raia huduma bora, amewaarifu kuwa serikali iliyojaa matumaini imerejea, akisema kwa takriban miaka mitatu miji ya Khartoum, Omdurman na Bahri iliyoko Kaskazini mwa Khartoum imekuwa uwanja wa mapambano.

Amesisitiza kwamba maeneo yote jirani yalikuwa yamezingirwa na wanamgambo na wapiganaji wakirusha makombora kuelekea mto Nile na mamilioni ya watu kukosa makaazi. Kulingana na Umoja wa Mataifa, kati ya mwezi Machi na Oktoba, watu milioni 1.2 walirejea Khartoum.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *