Uganda yaagiza kuzimwa kwa mtandao wa IntanetiUganda yaagiza kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti

Tume ya Mawasiliano ya Uganda imetuma barua kwa kampuni za kutoa huduma za intaneti ikisema hatua hiyo inalenga kupunguza kusambaa kwa taarifa potofu mtandaoni na kuzuia uchochezi wa vurugu wakati wa uchaguzi.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa yoyote kutoka serikalini kuhusu hatua hiyo ya kuzimwa kwa mtandao wa Intaneti. Maafisa walisema mamlaka hazikutaka “kumiliki” uamuzi huo.

Hii ni licha ya serikali kuahidi mara kadhaa kwamba intaneti haitazimwa wakati wa uchaguzi, ikisisitiza kupitia mtandao wa X tarehe 5 Januari kwamba madai ya kuzimwa kwa mtandao “si ya kweli na yanakusudia kuleta hofu kwa umma.”

Uganda iliwahi kuzima intaneti wakati wa uchaguzi wa mwaka 2021, uchaguzi uliokumbwa na madai ya wizi wa kura na ukandamizaji wa upinzani unaoongozwa na mwanamuziki aliyegeuka mwanasiasa, Bobi Wine, ambaye anawania tena urais mwaka huu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *