Mkutano wake wa kwanza ulifanyika London mapema mwaka 1946, na hadi leo ECOSOC bado ni kiini cha juhudi za Umoja wa Mataifa za maendeleo endelevu.

Wigo mpana na majukumu

ECOSOC ndilo jukwaa kuu la UN kwa majadiliano ya sera kuhusu masuala ya uchumi, jamii na mazingira, likiunganisha nchi wanachama, mashirika maalumu ya UN na wadau wengine. Majukumu yake makuu ni:

  • Kuratibu kazi za tume za kikanda, tume za kiutendaji, vyombo vya wataalamu na mifuko na programu za UN.
  • Kutoa mwongozo wa sera na msaada wa maendeleo unaogusa maisha ya kila siku ya watu.
  • Kusaidia majibu ya dharura, kusaidia nchi zinapona kutokana na migogoro, na kuratibu juhudi za kimataifa kupunguza umaskini, kuunda ajira na kulinda mazingira.
  • Kufuatilia mikutano mikuu ya UN ili kuhakikisha ahadi za ngazi ya juu hazipotei.

Kwa wale wasiofahamu mfumo wa UN, ECOSOC inajitofautisha kwa athari yake ya vitendo na jinsi inavyoshughulikia changamoto za kweli duniani.

Vipaumbele vya urais: “Kutekeleza kwa ufanisi zaidi”

Baraza limeweka vipaumbele vitano vya kisiasa:

  1. Kubadilisha kilimo na mifumo ya chakula ili kuimarisha ustahimilivu na kusaidia kutokomeza njaa.
  2. Kukuza ujasiriamali wa kidijitali na ushiriki wa vijana, kutumia kikamilifu uwezo wa idadi ya vijana.
  3. Hatua za tabianchi na ustahimilivu, hasa hatari zinazohusiana na maziwa ya barafu na mafuriko.
  4. Kurekebisha usanifu wa kifedha wa kimataifa ili uwe jumuishi zaidi na unaojibu mahitaji.
  5. Kutumia maadhimisho ya miaka 80 kutafakari jukumu na umuhimu wa ECOSOC katika siku za usoni.

Kubadilika na dunia inayobadilika

Tangu kuanzishwa kwake, ECOSOC limebadilika kukidhi muktadha wa dunia unaobadilika. Uanachama umeongezeka kutoka nchi 18 hadi 54 leo, huku Nchi Wanachama zikichaguliwa na Baraza Kuu kwa vipindi vya miaka mitatu vinavyoingiliana ili kuhakikisha uwiano wa kijiografia. Mageuzi ya Baraza Kuu katika muongo uliopita yameimarisha jukumu la ECOSOC kama msimamizi na mratibu wa mfumo wa UN, likiwezesha kutambua masuala mapya, kuhimiza ubunifu na kuunganisha vipengele vya kiuchumi, kijamii na kimazingira.

Mabango katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yakionesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs (Pichaya maktaba)

UN News/Abdelmonem Makki

Mabango katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa yakionesha Malengo ya Maendeleo Endelevu, SDGs (Pichaya maktaba)

Utekelezaji wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs)

Lengo kuu la sasa ni utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Maendeleo Endelevu, ramani ya kimataifa ya UN ya kutokomeza umaskini, kulinda sayari na kuhakikisha ustawi kwa wote. ECOSOC hutoa mwongozo wa kisiasa na usimamizi kupitia programu yake ya kazi ya kila mwaka, ikiwaleta pamoja mawaziri, maafisa wakuu, viongozi wa asasi za kiraia, wasomi na sekta binafsi.

Kiini cha kazi hii ni Jukwaa la Kisiasa la Ngazi ya Juu la Maendeleo Endelevu (HLPF), linalokutana kila mwaka chini ya uangalizi wa ECOSOC, likipitia maendeleo ya SDGs na ripoti za kitaifa za hiari kutoka serikali.

Maoni marefu ya chumba cha Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa (ECOSOC) wakati wa mkutano rasmi na wawakilishi walioketi kwenye dawati na mabango ya kimataifa kama vile Benki ya Dunia, IMF, WHO, WIPO, na IFAD.

UN Photo/Rick Bajornas

Muonekano wa Baraza la Uchumi.

Mara Chache kwenye vichwa vya habari

Tofauti na Baraza Kuu au Baraza la Usalama, mikutano ya ECOSOC mara chache huonekana kwenye vichwa vya habari, lakini inaonesha ugumu wa utawala wa kisasa wa dunia. Sehemu ya masuala ya kibinadamu huwaleta pamoja serikali na washirika kila mwaka ili kuimarisha uratibu wa majibu kwa migogoro ya muda mrefu na yenye gharama kubwa. Sehemu nyingine operesheni, uratibu na usimamizi huelekeza kazi za mashirika ya maendeleo ya UN, hupitia mapendekezo ya wataalamu kuanzia afya ya umma hadi taarifa za kijiografia, na kushughulikia masuala maalum ya nchi au kanda.

Daraja kwa asasi za kiraia

ECOSOC pia hufanya kazi kama daraja kati ya UN na ulimwengu mpana. Zaidi ya mashirika 3,200 yasiyo ya kiserikali yana hadhi ya mashauriano, yakipata njia rasmi ya kuchangia utaalamu na mitazamo ya uhalisia wa maeneo ya kazi. Mijadala maalum kwa vijana, wanasayansi, washirika wa maendeleo na wadau wengine inaakisi kwamba suluhu za kimataifa lazima ziwe jumuishi na zivanze zaidi ya serikali pekee.

Miaka 80, Lakini Bado Muhimu Zaidi

ECOSOC inapotimiza miaka 80 leo tarehe 23 mwaka wa 2026, dhamira yake kuu bado haijabadilika,  kukuza ushirikiano katika kufikia maendeleo ya pamoja ya kiuchumi na kijamii. Katika dunia yenye migogoro ikiwemo mabadiliko ya tabianchi, ukosefu wa usawa na dharura za kibinadamu, kazi yake tulivu ya uratibu na kujenga mwafaka inaendelea kuunda jinsi jumuiya ya kimataifa inavyoitikia.

Picha nyeusi na nyeupe ya mkutano wa kwanza wa Mkutano wa Pili wa Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa, ikionyesha wawakilishi kutoka nchi mbalimbali wakiwa wameketi kando ya meza kubwa iliyoinama na wasikilizaji wakiwa mbele.

Picha ya Umoja wa Mataifa

Baraza la Uchumi na Jamii la Umoja wa Mataifa

Ndani ya ukumbi wa ECOSOC

Ukumbi wa ECOSOC katika Makao Makuu ya UN, New York, ndio chumba kikuu cha mikutano ya Baraza, ikiwemo vipindi vya ngazi ya juu na majadiliano ya mawaziri. Ukumbi huu, uliozinduliwa mwaka 1952 na kubuniwa na mbunifu Sven Markelius, ulifanyiwa ukarabati mkubwa mwaka 2013.

Ukumbi una vipengele vya kiishara kama mapazia makubwa Dialogos, yakionesha mazungumzo na majadiliano ya mawazo wa kiini cha ECOSOC kama jukwaa la kujenga mwafaka. Mojawapo ya sifa zake za kipekee ni dari yake isiyokamilika; mabomba na mifereji iliyoachwa wazi inaashiria kwamba kazi ya Umoja wa Mataifa na maendeleo ya kiuchumi na kijamii haikamiliki kamwe, bali ni juhudi ya pamoja inayoendelea.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *