SHINYANGA: DIWANI wa Kata ya Malunga Manispaa ya Kahama mkoani Shinyanga, Ahamed Haruna ametoa miezi sita kwa wananchi waliofunga mikataba kwenye eneo la soko kwa ajili ya ujenzi wa vibanda na kuvitelekeza takribani miaka 10 wavikabidhi mara moja kwenye uongozi na wasiendelee kuvishikilia kama vimewashinda.

Haruna amesema hayo kwenye mkutano wa hadhara uliokuwa na lengo la kuwashukuru wananchi kumchagua na kuwatambulisha rasmi kuwa ameanza kazi ya utekelezaji wa IIani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) nakupunguza migogoro angalau kwa asilimia 70.

Haruna amesema eneo hili la soko ameanza kulifuatilia ili kufahamu linamilikiwa na nani kama siyo halmashauri au eneo la Jumuiya ya Umoja wa vijana wa CCM ajue kwani kuna vibada vimejengwa takribani miaka 10 na vimetelekezwa nakuwa vichaka na dampo la kutupia uchafu.

“Hatuwezi kuwa na soko lisilokuwa na manufaa (butu) na hili suala sitalifumbia macha ninatoa muda wa miezi sita tu kwa hekima kuhakikisha wenye vibada wachukue hatua,” amesema Haruna.

Haruna amesema eneo hili la soko atahakikisha lina boreshwa vizuri vibanda hivi kwa wasio viboresha watapokonywa na kupewa watu wengine muda ukifika bila kuona juhudi zozote na kutawekwa taa nyakati za usiku ili wafanyabiashara waweze kuuza bila kutumia taa zao ndogo au tochi.

Haruna amesema soko linatakiwa liwepo na liwanufaishe watu wote kwani inasikitisha kuona kata hii haina soko lakini maeneo mengine yapo na wakazi wake wanauza bidhaa bila wasiwasi wowote.

Baadhi ya wakazi wa kata hiyo akiwemo Veronika Fabian na Katemya Jumanne wamesema kweli eneo la soko limekuwa likiogopesha hasa ikianza nyakati za usiku wengi wanahofia kuwa ni maficho ya wahalifu au wanyama wakali kama vibanda vyote vikiboreshwa watakaa kwa amani kuuza bidhaa zao.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *