
Nchini Uganda, serikali inakataa shutuma za ukandamizaji wa kisiasa. Katika taarifa iliyotolewa Januari 27, 2026, Waziri wa Habari alitetea kukamatwa kwa watu na kuzimwa kwa huduma yaintaneti, akisema kwamba alichukua hatua dhidi ya “magenge ya wahalifu” yanayoshutumiwa kwa kujaribu kusababisha mzozo baada ya uchaguzi.
Imechapishwa:
Dakika 2 Wakati wa kusoma
Matangazo ya kibiashara
Taarifa hiyo imekaribisha “mazingira” ambamo uchaguzi Januari 15 ulifanyika, licha ya baadhi ya matukio, na kupongeza chama tawala kwa “ushindi wake,” pamoja na rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa kwake tena. Hii ilikuwa njia ya kuthibitisha uhalali wa uchaguzi, huku upinzani ukipinga matokeo na ukosoaji ukiongezeka kuhusu hali ya usalama.
Katika taarifa iliyotolewa siku ya Jumanne, Waziri wa Habari wa Uganda alifutilia mbali shutuma za ukandamizaji wa kisiasa, akihalalisha watu kukamatwa na kuzimwa kwa huduma ya intaneti kama mapambano dhidi ya “magenge ya wahalifu” ambao, kulingana naye, wanajificha nyuma ya harakati za kisiasa ili kuchochea machafuko.
“Huu si ukandamizaji wa kisiasa, ni kudumisha utulivu wa umma dhidi ya magenge”: hii ndio hoja kuu iliyotolewa na Chris Baryomunsi kutetea mkakati wa usalama wa serikali ya Uganda baada ya Uchaguzi Mkuu wa Januari 15. Waziri huyo aliwasifu watu ambao “walibaki watulivu” huku akitaja “matukio yasiyoeleweka” ambayo, kulingana naye, yangeweza kutishia utulivu wa umma.
Katika taarifa hiyo, alimpongeza Rais Yoweri Museveni kwa kuchaguliwa tena na chama tawala, NRM, kwa “ushindi wake wa mkubwa.” Utetezi uliolenga kuthibitisha uhalali wa uchaguzi, wakati ambapo upinzani unapinga matokeo na ukosoaji unaongezeka kuhusu hali ya usalama.
“Magenge” yanayojificha nyuma ya siasa, kulingana na serikali “Magenge haya ni akina nani”? Kulingana na Baryomunsi, haya ni makundi ya wahalifu “yaliyojificha kama wanaharakati wa kisiasa,” yaliyohamasishwa “kuvuruga amani” na kuchochea makabiliano na polisi. Katika taarifa hii, alitaka kutafautisha kati ya uanaharakati, uchochezi, na uhalifu uliopangwa kimakusudi.
Waziri huyo pia anadai kuwa na ushahidi—ikiwa ni pamoja na picha—zinazoonyesha viongozi wa upinzani wakiwafundisha wafuasi jinsi ya “kuvishinda” vikosi vya usalama. Anadai kwamba washukiwa tayari wamekamatwa na kwamba wengine watakamatwa “kwa mujibu wa sheria.”
Kinyume na hali hiyo, serikali inaishutumu Jukwaa la Umoja wa Kitaifa (NUP), chama cha Bobi Wine, kwa kuchochea vurugu hizi. Upinzani unakanusha shutuma hii, badala yake ukidai kwamba wanaharakati wake wanalengwa na vikosi vya usalama.