#HABARI: Ndege ya abiria imeanguka kaskazini mwa Colombia na kuwaua watu wote 15 waliokuwemo, shirika la ndege la serikali la nchi hiyo , limethibitisha, katika taarifa shirika hilo limesema ndege yake aina ya Beechcraft 1900 ilipata ajali mbaya.
Mabaki ya ndege hiyo sasa yamepatikana katika eneo la milima huku orodha rasmi ya abiria ikijumuisha mbunge Diógenes Quintero Amaya na Carlos Salcedo wanaogombea uchaguzi ujao wa bunge.
Shirika la ndege la nchi hiyo limesema mawasiliano na ndege hiyo yalikatika dakika 11 kabla ya muda uliopangwa wa kutua katika mji wa Ocaña, karibu na mpaka wa Venezuela, mchana siku ya Jumatano.
Kwa mujibu wa shirika hilo, ndege iliondoka katika mji wa Cúcuta, takribani kilomita 100 (maili 62) kaskazini-mashariki mwa Ocaña ikiwa imebeba abiria 13 na wahudumu wawili wa ndege.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.