China imewanyonga watu 11 waliohusishwa na uhalifu uliopangwa nchini Myanmar leo Alhamisi, Januari 29, wakiwemo “wanachama muhimu” waliohusika katika vituo vya utapeli mtandaoni, shirika la habari la Xinhua limeripoti.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

“Adhabu hiyo ya kifo imefanywa na mahakama katika Jiji la Wenzhou, Mkoa wa Zhejiang, mashariki mwa China, baada ya kupokea idhini kutoka kwa Mahakama Kuu ya Watu,” shirika la habari la serikali limesema. 

Mahakama ya mkoa wa Zhejiang iliwahukumu wanachama wa familia ya Ming mwezi Septemba mwaka jana kwa makosa mazito yaliyohusisha mauaji, kuwazuia watu kinyume cha sheria, ulaghai, pamoja na kuendesha nyumba za kamari haramu.

Milki yao ya ulaghai iliporomoka mwaka 2023 baada ya wanachama wake kukamatwa na kukabidhiwa kwa China na makundi ya kijeshi ya kikabila yaliyokuwa yameuteka mji wa Laukkaing katika muktadha wa vita vya wenyewe kwa wenyewe vinavyoendelea Myanmar.

Kwa miaka mingi, mitandao ya ulaghai nchini Myanmar imewanasa maelfu ya raia wa China, na pia bara la Afrika halijasazwa, ambao ni miongoni mwa mamia ya maelfu ya watu waliotekwa au kusafirishwa kwa nguvu hadi katika kambi hizo, ambako walilazimishwa kuwalaghai watu wa nchi za nje.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *