#HABARI: Kampuni kubwa ya mafuta ya nchini India (Indian Oil Corporation Limited) imeonesha nia ya kuwekeza nchini Tanzania katika sekta ya usambazaji wa mafuta na gesi.
Nia hiyo imebainishwa wakati wa kikao kati ya uongozi wa kampuni hiyo na ujumbe wa Tanzania ukiongozwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Salome Makamba, pembezoni mwa maadhimisho ya Wiki ya Nishati ya India (IEW 2026) yanayoendelea katika Jimbo la Goa.
Mkurugenzi wa Mipango na Biashara wa kampuni hiyo, Suman Kumar, ameeleza kuwa ukuaji wa haraka wa uchumi na ongezeko la watu nchini Tanzania unatoa fursa kubwa kwa soko la nishati, hususan katika uchakataji na usambazaji wa gesi ya mitungi (LPG).
Kwa upande wake, Mhe. Salome amewakaribisha wawekezaji hao na kuwahimiza kufungua matawi nchini ili kuongeza ushindani na uhakika wa upatikanaji wa nishati kwa gharama nafuu.
Uwekezaji huu unatarajiwa kuendana na msukumo wa Serikali ya Awamu ya Sita wa kukuza matumizi ya nishati safi ya kupikia na kuimarisha uchumi wa taifa.
Maadhimisho hayo ya Wiki ya Nishati yanayohitimishwa Januari 30, 2026, yamekuwa jukwaa muhimu kwa Tanzania kujitangaza na kuvutia teknolojia pamoja na mitaji kutoka kwa wadau wa kimataifa katika sekta ya mafuta na gesi.
Powered by #MCHEZOSUPA
JINSI YA KUSHIRIKI MCHEZO SUPA:
–
Tuma 1000 kupitia Airtel Money, Tigo Pesa, M – Pesa, Halopesa, kwenda namba ya kampuni 222223 kumbukumbu namba ni 777 au weka neno ITV.
#ITVDigital #ITVUpdates #ITVTanzania
Follow @itvtz @radioonetanzania
@capitaldigitaltanzania.