Nchini Côte d’Ivoire, Mahakama ya mwanzo ya Abidjan imemhukumu Mahamadou Gassama kifungo cha miaka mitatu jela siku ya Ijumaa, Januari 30, 2026, kwa “kumtukana rais” na “kusambaza maneno ya machafu mtandaoni.” Afisa huyu wa Mali kutoka Baraza la Kitaifa la Mpito (CNT) alikamatwa mnamo mwezi Julai 2025, kufuatia ziara ya kibinafsi nchini Côte d’Ivoire.

Imechapishwa:

Dakika 1 Wakati wa kusoma

Matangazo ya kibiashara

Na mwandishi wetu mjini Abidjan, Bineta Diagne

Mahakama ilimhukumu Mahamadou Gassama kifungo cha miaka mitatu jela na kuamuru alipe faini ya faranga za CFA milioni 5. Mbali na hukumu hizi, alipigwa marufuku kuingia Côte d’Ivoire kwa miaka mitatu. Aliposikia hukumu hiyo, Mahamadou Gassama alisangaa, kama vile familia yake na marafiki zake waliokuwa wamesafiri kutoka Bamako kuja kumuunga mkono. Wakili wake, Ismaila Konaté, alielezea masikitiko yake.

Mahamadou Gassama anatuhumiwa kutoa matamshi mwaka wa 2022, wakati wa kilele cha mgogoro kati ya Côte d’Ivoire na Mali, kuhusu wanajeshi Côte d’Ivoire waliokamatwa Bamako. Hasa, alitoa taarifa ambapo mjumbe huyu wa Baraza la Kitaifa la Mpito alitangaza: “Rais wa Côte d’Ivoire ni adui wa Mali.”

Mahakamani mnamo Januari 9, Mahamadou Gassama alikiri matamshi hayo na kuomba msamaha. “Sikujua inaweza kuwa ya kuumiza,” alisema. Mwanasiasa huyo alidai kuwa amemwandikia barua Rais waCôte d’Ivoire Alassane Ouattara kuomba msamaha.

Kitendo hiki cha kuomba msamaha hakikushawishi upande wa mashtaka. Mwendesha mashtaka aliona msamaha huo “umechelewa” na “haukubaliki kwa mtu wa hadhi yake.” Wakati wa hoja zake za mwisho, mahakama ilikumbusha kuwepo kwa kampeni ya uhamasishaji inayolenga kuwatia moyo raia kutumia lugha inayowajibika kwenye mitandao ya kijamii.

Mawakili wa Mahamadou Gassama wanabaini kwamba uamuzi wa mahakama ni “mzito, na mkali.” Mmoja wao, Ismaila Konaté, alielezea masikitiko yake. Ingawa wanakubali kwamba kosa la mteja wake “ni kubwa,” yeye na mawakili wenzake wa upande wa utetezi “wanasadiki kwamba mazingira ya kesi hiyo, muktadha wake, na hasa msamaha wa mara kwa mara wa Bw. Gassama haupaswi kumhukumu adhabu kali kama hiyo.” Utetezi una siku 20 za kukata rufaa.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *