
Hiki ni kipindi kinachohusisha mahojiano ya kusisimua na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya Japani. Wakati huu, tunakuletea riwaya kuhusu simulizi ya “Nipo kwa ajili yako” iliyoandikwa na Totoki Naoko. Simulizi hii inagusa hisia za kipekee za mwanamke anayerudi kazini baada ya likizo ya uzazi.
Aidha, utasikiliza namna watangazaji wetu wanavyozamia gumzo za kuvutia zitakazokuacha ukivunjika mbavu. Hatimaye, kipindi kitafikia ukingoni baada ya sisi kutangamana nawe msikilizaji kwa kusoma ujumbe wako. Usikose kusikiliza!
Kipindi hiki kilitangazwa Julai 28, 2024.