Mkuu wa Wilaya ya Morogoro Mussa Kilakala amewataka madiwani kuhakikisha kabla ya kubuni vyanzo vipya vya mapato wahakikishe vyanzo vingine vinafanya vizuri katika ukusanyaji wa mapato.

Akizungumza katika baraza la Madiwani Manispaa ya Morogoro Kilakala amesema ni muhimu kuhakikisha vyanzo vilivyopo kwa sasa vinafanya vizuri huku akiwashauri wanapo buni miradi mingine basi iwe rafiki kwa wananchi nasiyo kuwaumiza zaidi.

Kwa upande wake Mstahiki Meya wa Manispaa ya Morogoro Khalid Matengo amesema kuelekea Manispaa hiyo kuwa jiji wanaendelea kuziba mianya na upotevu wa mapato ambayo ndio msingi imara wa kufikia matarajio ya kuwa jiji.

Naye Mwenyekiti wa chama cha Mapindizi CCM Wilaya ya Morogoro Fikiri Juma amezihimiza taasisi zote na wadau wanaopaswa kuhudhuria katika baraza la madiwani wawe na utamadumi wa kuhudhuria ili kusikiliza kile kinachojadiliwa ili kwenda kuwatumikia wananchi kwa ufanisi.

(Feed generated with FetchRSS)

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *