Mazungumzo ya Amani ya Ukraine yaahirishwa hadi JumatanoMazungumzo ya Amani ya Ukraine yaahirishwa hadi Jumatano

Hayo ni kwa mujibu wa Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ambaye hata hivyo hakutoa sababu ya kucheleweshwa kwa mazungumzo hayo.

Tangazo hili linajiri siku moja baada ya mjumbe wa ngazi ya juu wa Rais Vladimir Putin kufanya mazungumzo ya kushtukiza na maafisa wa Marekani huko Florida bila ya uwepo wa Ukraine.

Mazungumzo hayo ya pande tatu yanatarajiwa kufanyika Abu Dhabi tarehe 4 na 5 Februari, ingawa Marekani na Kremlin bado hawajathibitisha rasmi tarehe hizo.

Washington inasisitiza kuwa iko karibu kufikia makubaliano ya kumaliza vita ambavyo vimekuwa vya umwagaji damu zaidi barani Ulaya tangu Vita Kuu ya Pili ya Dunia. Hata hivyo, suala la mipaka bado limekwama, huku Urusi ikitaka udhibiti kamili wa jimbo la Ukraine la Donbas, lakini Ukraine inapinga vikali mkataba wowote wa kuilazimisha iachie ardhi yake.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *